HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 22, 2016

ROSE NDAUKA, BARAKA DA PRINCE KUMSINDIKIZA MC PILIPILI KWENYE TAMASHA LA KRISIMAS.



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa kizazi kipya Baraka Da Prince kwa pamoja na Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Rose Ndauka wamesema kuwa wamejiandaa vema kumsindikiza Mchekeshaji maarufu nchini , Emanuel Matebe a.k.a Mc Pilipili katika Tamasha la Chrismass la kids Festival litakalofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Desemba 25 na 26 mwaka huu.

Wasanii hao pia Desemba 26 mwaka huu watatoa burudani nyingine kama hiyo katika ukumbi wa 
Royal Village na kuwapa fursa watu wa Dodoma kupiga picha na Tuzo aliyoipata Mc.Pilipili ya
Mshereheshaji bora wa mwaka 2016.

Akizungumza hivi karibuni na Ripota wa Globu hii,Muigizaji nguli Rose Ndauka alisema kuwa 
tamasha hilo litakuwa la kipekee katika mkoa wa Dodoma ambapo ataweza kupanda jukwaani 
pamoja na Mchekeshaji huyo na kutoa burudani ya aina yake. 

Alisema pia ataamua kuongea ukweli juu ya uhusiano wake na Mc Pilipili katika tamasha hilo kwani 
watu wengi wamekuwa wakiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya ukaribu waliokuwa 
nao. 

"Nataka kuwaambia watu wangu wa Dodoma kule kwa kina Mc.Pilipili mkae tayari kwa ujio wangu 
kwani siku hiyo ndio itakuwa siku yangu maalum ya kupanda jukwaani na Mc.Pilipili katika 
kuhakikisha nina wavunja mbavu mashabiki zangu pia naombeni mjitokeze kwa wingi kuitikisa siku hiyo kwenye mji Dodoma na viunga vyake,"alisema 

Kwa Upande wake Emanuel Matebe a.k.a Mc Pilipili alisema tamasha hilo litakuwa ni tamasha la ainayake kwani litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini wa muziki wa kizazi kipya pamoja na waigizaji wakiwemo Baraka da Price,Rose Ndauka ,Katarina Karatu pamoja na Casto . 

Alisema katika tamasha hilo Decemba 25 mwaka huu watoto wataweza kuingia kwa kiingilio cha 
shilingi 2000 huku wakubwa sh.5000 huku katika tamasha la Desemba 26,kutakuwa na kiingilio cha 
VIP ikiwa 30000 na kawaida 10000.

"Nawakaribisha ndugu zangu wa Dodoma katika matukio haya mawili siku hiyo itakuwa siku ya 
pekee kwangu kuonyesha kipaji changu nyumbani hivyo nitahakikisha nawatendea haki ipasavyo 
huku nikirudisha tuzo ya Mshereheshaji bora nyumbani niliyopewa katika tuzo za Insta Award 
ambayo mashabiki zangu watapata fursa ya kupiga nayo picha,"alisema

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad