Jeneza lililobeba mwili wa mpiga picha maarufu Marehemu Mpoki Bukuku ukiwa katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu ya kutoa heshima za mwisho
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mpoki Bukuku wakati wa kuagwa kwa mwili huo.
Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo pamoja na Muwakilishi wa Bloggers, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi katika Msiba wa Mpoki Bukuku, viwanja vya Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar.
Baadhi ya waombolezaji wa wakiwa kwenye shughuli ya kuagwa kwa mwili wa marehemu Mpoki Bukuku katika uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu.














No comments:
Post a Comment