HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 15, 2016

MROPE, AHMADA SEIF WASHUSHWA HADI LIGI DARAJA LA KWANZA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMATI ya waamuzi Nchini imewashusha waamuzi Rajab Mrope na Ahmada Seif kutoka ligi kuu mpaka ligi daraja la kwanza. Katika ratiba ya ligi kuu iliyotoka waamuzi hao hayakuwepo majina yao, na rasmi sasa yameonekana kwenye ratiba ya ligi daraja la kwanza.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi (kamati ya masaa 72) kuwaondoa kwenye ratiba ya ligi kuu na shauri lao kulirudisha kwenye kamati ya waamuzi.

Mrope aliondolewa kwenye ratiba hiyo baada ya kuonyesha udhaifu kwenye mechi ya Mbeya City dhidi ya Yanga kwa kutokuwa na maamuzi sahihi kwa kulikubali goli, kuliktaa na mwisho kulikubali tena mechi iliyomalizika kwa Mbeya City kushinda 2-1.

Ahmada Seif aliondolewa kwa kosa la kutokuhimili mchezo wa African Lyon dhidi ya Mbao Fc kwa kutoa penati iliyozua utata kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa Lyon kushinda 3-1.

Kamati ya waamuzi bado haijatoa maamuzi ya Mwamuzi Martin Saanya na Samuel Mpenzu ambao nao pia waliondolwa kwenye ratiba ya ligi kuu Vodacom..


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad