
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh,Amos Makalla asema wananchi wanalalamikia urasimu , Rushwa na ubadhirifu
MKuu wa Mkoa wa Mbeya Amewataka watumishi wa umma kuwajibika na kutoa huduma kwa wananchi kwa kiwango cha juu ili wananchi wazione ofisi za umma kimbilio Lao
Hayo ameyasema Leo katika maadhimisho ya siku ya maadili mkoani Mbeya ambako maadhimisho hayo yamefanyika kikanda Mkoani mbeya.
Amesema lazima watumishi wa umma wabadilike na kuacha kutumia muda mwingi kufanya shughuli binafsi wakati wa kazi na pia watumishi waache kauli za njoo kesho kufanya hivyo Ni kutengeneza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali.
Aidha urasimu wa maamuzi ni kiashiria cha kutaka rushwa Baadhi ya watumishi huweka urasimu mkubwa katika kutoa maamuzi kwa lengo la kutaka rushwa na amewataka watumishi wa aina hiyo kubadilika mara moja.
Rc Makalla pia Amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika mapambano ya Rushwa kwani kazi hiyo si ya Takukuru tu bali ni wananchi wote ili kutokomeza rushwa.


Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla Kulia, Akijumuika na baadhi ya wadau walio hudhuria hafra hiyo ya maadhimisho ya siku ya maadili mkoani Mbeya.

Baadhi ya wageni waalikwa na baadhi ya wadau kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makini.
No comments:
Post a Comment