Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Sakata la mchezaji Zahoro Pazi aliyesajiliwa na timu ya Mbeya City limefikia tamati leo baada ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutuma hati yake ya uhamisho wa kimataifa (ITC) kwenda katika shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Mbeya City walishindwa kumtumia mchezaji huyo ingawa ni mtanzania kwa kuwa hakuwa na hati ya uhamisho kutoka katika timu yake ya awali kuchelewesha kumtumia kwa mchezaji huyo.
Zahoro aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili kwa sasa anaweza kuitumikia klabu yake hiyo mpya ya Jijini Mbeya baada ya ITC yake kuwasili TFF


No comments:
Post a Comment