Na Antony John wa Globu Ya Jamii
Wafanya biashara mbalimbali katika soko la Karikoo wamesema hali ya kibiashara bado imekuwa ngumu katika kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.
Wakizungumza na Globu ya Jamii wafanya biashara hao wamesema hali ya kibiashara imekuwa ngumu kwa kuwa watu wengi hawaendi kununua bidhaa sokoni hapo kwa sababu wanaogopa ukubwa wa bei katika kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu.
Wafanya biashara hao wamewataka wateja kutokuwa na wasiwasi wa kwenda kununua bidhaa sokoni hapo kwa kuwa bei bado ipo vile vile hazijaongezeka katika kipindi hiki.
Aidha wafanya biashara hao waliwaomba wateja watakao kwenda kununua bidhaa Sokoni hapo wasiishie nje ya Soko na badala yake kwenda kununua bidhaa ndani ya Soko hilo kwa kuwa bei za Ndani ya Soko ni rahisi kuliko za nje.
Mfanya biashara wa Soko la Kariakoo Alhaji Kabula akizungumza na Globu ya Jamii kuhusiana na bei ya Mchele Leo hii katika Soko hilo la Kariakoo.Mfanyabiashara wa nyama Zacharia Zacharia katika Soko la Karikaoo akizungumza na Michuzi Tv juu ya hali ya bei ilivyokuwa kwa kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.

No comments:
Post a Comment