Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt Harrison Mwakyembe amezindua wiki ya utoaji huduma kwa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi wa wa wiki ya utoaji huduma na upokeaji wa malalamiko kutoka kwa wananchi katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya maadili Disemba10 , Dk. Mwakyembe amesema Serikali haitomfumbia macho mtumishi yeyote anayekiuka maadili na kutumia vibaya nafasi aliyonayo.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa watendaji watakaochelewesha utoaji haki na huduma kwa wananchi Serikali haitowaonea haya kuwawajibisha ipasavyo.
Taasisi saba za umma zinashiriki kwenye utoaji wa huduma ambazo ni ofisi ya rais - menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, takukuru, sekretariat ya maadili ya viongozi wa umma, ppra, naot, tume ya utumishi wa umma na tume ya haki za binadamu.
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau mbalimbali kwenye uzinduzi wa wiki ya kutoa huduma kwa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akizungumza kwenye Uzinduzi wa wiki ya kutoa huduma kwa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.


.Afisa Mtafiti wa shughuli za mfuko wa Taifa wa bima ya Afya, Shani Mussa akizungumza na Mwananchi alieetembela banda la (NHIF)katika uzinduzi wa wiki ya kutoa huduma kwa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Harrison Mwakyembe akishirikiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki kuzindua rasmi wiki ya kutoa huduma kwa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti Lello,
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Harrison Mwakyembe akifrahia jambo na Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti Lello, leojijini Dar es Salaam.
.Afisa Mtafiti wa shughuli za mfuko wa Taifa wa bima ya Afya, Shani Mussa akizungumza na Mwananchi alieetembela banda la (NHIF)katika uzinduzi wa wiki ya kutoa huduma kwa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment