Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuhusu utekelezaji wa miradi ya miundombinu alipowatembelea ofisini kwao.
Muonekano wa barabara ya Changarawe ya Loliondo – Mto wa Mbu KM 218 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Arusha.
Mkazi wa Kijiji cha Sale, Bw. Michael Nagwianye akitoa maoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu KM 218 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Serikali
imesema ipo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Loliondo-
Mto wa Mbu yenye urefu wa KM 218 itakayojegwa kwa kiwango cha lami ili
kurahishisha usafiri na usafirishaji wa mizigo kwa wananchi wa mikoa ya
Mara, Manyara, Arusha na Mwanza.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
katika kijiji cha Sale, wilayani Ngorongoro mara baada ya kukagua barabara hiyo
ambayo ni kiungo kati ya mikoa hiyo minne na nchi jirani ya Kenya.
"Tumeshatangaza
Zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, mapema mwakani zitafunguliwa ili
kumpata mkandarasi ambae atajenga barabara hii kwa kiwango kilichobora",
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha,Waziri
huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara hiyo utatekelezwa kwa awamu mbalimbali
ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa barabara ya kutoka katika kijiji
cha Waso - Sale yenye urefu wa KM
49.
Ameongeza
kuwa barabara hiyo ikikamilika itaungana na ile ya Makutano-Nata yenye urefu wa
KM 50 iliyopo Wilaya ya Butiama, mkoani Mara na itasaidia kupunguza kero ya
usafiri na kufungua mikoa hiyo kibiashara kwa wakazi wa maeneo hayo.
Amewataka
wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa mkandarasi atakayepata zabuni
hiyo ili kumrahisishia kumaliza mradi huo kwa wakati na viwango
vinavyokubalika.
Kwa
upande wao wakazi wa Kijiji cha Sale wamemuelezea Waziri Changamoto
wanazozipata katika barabara hiyo na kuiomba Serikali kuharakisha mradi huo
kwani utasaidia kuongeza pato katika Sekta ya Utalii na kurahisisha huduma za
kijamii.
“Barabara
hii ni ya muhimu sana kwani tumeteseka kwa muda mrefu, huduma za kijamii kama
kumsafirisha kutoka nyumbani mpaka kwenye kituo cha afya ilikuwa ikituchukua
muda mrefu kutokna na ubovu wa miundombinu”, amesema Bw. Elias Badiani.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano


No comments:
Post a Comment