Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSANII wa muziki wa kizazi Kipya 'Bongo Fleva' Abbas Bakari 'Abby skills' amewashukuru mashabiki wake kwa kuupokea wimbo wake wa Averina na kusema kuwa wakae tena kwa mkao wa kula kwani kuna nyimbo saba zipo tayari.
Abbyskills ameachia wimbo wa Averina mwanzoni mwa Novemba na umeweza kumpatia show kadhaa na tayari ameanza kupata mafanikio kwa kupitia wimbo huo aliowashirikisha wasanii Ali Saleh Kiba 'Ali kiba' na 'Mr Blu'.
Amesema kuwa, menejiment yake ambayo kwa sasa yupo chini ya lebo ya KING STUDIO amejipanga kuhakikisha anazidi kuwapa burudani mashabiki wake na zaidi nyimbo zipo tayari zinasubiri kupakuliwa tu.
Abbyskills ameendelea na kusema kuwa , ujio wa wimbo wa Averina umekuwa na manufaa makubwa sana kwake kwani ndani ya mwezi mmoja na nusu ameweza kupata show ikiwemo FIESTA ya mwaka huu iliyofanyika Novemba 05.
Kwa sasa Abbyskills anajiandaa kuachia nyimbo mpya itakayotarajiwa kutoka Februari 2017 na mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani atakuja na kikubwa zaidi ya Averina.
No comments:
Post a Comment