
Ndege ya shirika la Precision Air ikiruka kutoka uwanja mdogo wa Seronera ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoa wa Mara, Muda mfupi baada ya kushusha watalii
43 kutoka nchi Afrika Kusini iliyowachukua katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere hatua inayoelezwa kuokoa muda na kupunguza
gharama.

Ndege
ya shirika la Precision Air ikiwa tayari imetua katika uwanja wa
Seronera ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoa wa Mara ikiwa na
watalii 43 kutoka nchi Afrika Kusini iliyowachukua katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hatua inayoelezwa kuokoa muda na
kupunguza gharama.

Abiria
wakishuka kutoka kwenye ndege ya shirika la Precision Air ambayo
imeanza safari za moja kwa moja kutoka jijini Dar es Salaam na Zanzibar
hadi kwenye hifadhi hiyo.

Watalii wakifurahi baada ya kutua salama kwenye uwanja wa Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Meneja
Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(katikati)akiwa katika
picha ya pamoja wa wafanyakazi wa shirika la Precision Air,kulia kwake
ni Kapteni Benjamini Maluli na kushoto kwake ni Murtazir Ghulamhusein.

Watalii wakipata picha ya pamoja ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Meneja
Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akifafanua umuhimu wa ndege kubwa
za abiria kwenda moja kwa moja kwenye hifadhi za taifa kutakavyoinua
sekta ya utalii nchini.

Makundi makubwa ya wanyama aina ya Nyumbu ni miongoni mwa vivutio ndani hifadhi ya Serengeti.

Tembo wenye miili mikubwa wakiwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti.

Fisi wakijipooza joto kwenye dimbwi la maji.



Wafanyakazi wa Sence of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa tayari kuwapokea wageni wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment