Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei Tanzania
kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Clara Salon &
Boutique imefungua duka kubwa liitwalo “Clara Smartphone Shop” katika Jiji la
Mwanza. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya
mikakati yake ya kujitanua kibiashara nchini.
Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Clara, katika Jiji la Mwanza
kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya
watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.
“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii tuko
Mwanza. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Mwanza na miji ya
jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu. Tunaamini kuwa
Clara Salon & Boutique wana jina kubwa katika Jiji la Mwanza na hivyo
itatusaidia sisi kutimiza lengo letu, anasema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang(kulia) na Mkurugenzi wa Clara Huawei Smartphone Brand Shop, Clara Mwasa wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Huawei
inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza
kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Clara. Milango iko wazi kwa yeyote
anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.
Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda ya Ziwa,
Mkurugenzi huyo alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na
nyinginezo, katika soko la simu nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang(katikati) akiwaonyesha wateja walihudhuria uzinduzi wa Duka la Clara Huawei Smartphone Brand Shop lililozinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.Kulia ni Mkurugenzi wa Duka hilo, Clara Mwasa.
Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia, akifafanua
zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa, ikilinganishwa na
simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na simu hiyo kama
matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na nyingine nyingi.
Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Mwanza. Kuanzia sasa
wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati.
Tunaanza na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua
kuitumia ataipenda kwa ubora wake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato
wake wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo
yake ili kupambana na soko la mawasiliano.
No comments:
Post a Comment