Na Lulu Mussa,
Sumbawanga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake siku
ya leo Waziri Makamba ameshuhudia uharibifu mkubwa wa mazingira hususan
pembezoni mwa ziwa Rukwa.
Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000
kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo
hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.
"Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina
hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na
kandokando ya ziwa, na ulishaji wa mifugo katika Vyanzo vya maji" Makamba
alibainisha
Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba
ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na
kanuni za matumizi ya maeno hayo zitaandaliwa ili kunusuru Ziwa Rukwa.
Pia, wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa
zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalum
'beacons' ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwa zoezi hili lifanyike haraka.
Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko
yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa
kiwango kikubwa. "nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa"
Makamba aliongezea.
Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani
itakuwa lazima kwa wanafunzi wa Primary na Sekondari kuwasili na miti na kutakiwa
kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta
wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha
uoteshaji wa miti.
Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali za dini na
wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani, na kuahidi
kugharimia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo na kusisitiza agenda ya
Mazingira iwepo.
Mkoani Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza
na wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Nankanga
ambapo wakazi wa maeneo hayo wamempongeza kwakua toka kijiji hicho kianzishwe
mwaka 1974, Waziri Makamba ndio amekuwa mgeni wa kwanza Kitaifa kuwatembele.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akiwa pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wakielekea kutembelea
fukwe za ziwa Rukwa zilizoharibiwa vibaya
Sehemu ya wakazi wa Nankanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na
Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Waziri akiwahimiza
juu ya kutuza rasilimali za Mazingira.
Mifugo ikichungwa pembezoni mwa Ziwa Rukwa, ambapo Waziri Makamba amegiza
shughuli za aina hiyo kufanyika mita 200 kutoka kwenye chanzo cha maji
Sehemu ya Viongozi wa dini, siasa na wazee wa Mkoa wa Rukwa wakimsikiliza
Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani)
alipokutana nao na kusisitiza amani na Hifadhi ya mazingira.
No comments:
Post a Comment