HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 19, 2016

TANZIA: MKONGWE WA MUZIKI WA TAARAB AFARIKI DUNIA LEO

Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali akakata roho. Taarifa kamili tutawaletea mara tu tutapozipata.

MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA

Kipindi cha Danga Chee cha Michuzi TV kilihojiana na marehemu Bi Shakila miezi sita iliyopita, yakiwa  ni mojawapo ya mahojiano ya mwisho kabla malkia huyo mwenye sauti nyororo kututoka. Sikiliza hapa chini:

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad