HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 2, 2016

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANIBARI WAISHIO BOSTON, MAREKANI

Na Mwandishi wetu Boston
Makamu wa Kwanza Mstaafu wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amemaliza awamu ya pili ya ziara zake za Kimataafa nchini Marekani iliyoanza wiki mbili zilizopita.
Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) alikamilisha ziara yake hiyo tarehe 30 Julai kwa kuzungumza na Wazanzibari kwenye Mkutano uliofanyika katika jimbo la Massachusetts.
Mgeni huyo rasmi alikaribishwa kwa risala ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio katika jiji la Boston kulikofanyika mkutano huo iliyosomwa na Bwana Mohammed Lali, iliyoelezea imani yao juu ya uongozi wa Maalim Seif katika mapambano ya kupigania haki sawa na demokrasia Visiwani Zanzibar.
Akijibu risala hiyo, Mwanasiasa huyo alielezea shukrani zake za dhati kwa imani ya Wazanzibari juu uongozi wake na kuwahakikishia kuwa haki yao itapatikana.
Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad