HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 20, 2016

BI. SHAKILA KUZIKWA LEO SAA 10 ALASIRI MAKABURI YA UWANJA WA NINJA, MBAGALA CHARAMBE JIJJINI DAR

Kwa mujibu wa familia marehemu Bi. Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es salaam 

Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.

Bi Shakila alifariki jana baada ya kuanguka nyumbani kwake mara baada ya kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu wa binti yake, Shani, mkongwe huyu wa taarabu hakuwa anaumwa wajati mauti yanamkuta.

KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad