Imekuwa ni kawaida kwa makampuni ya simu za Mikononi za Tanzania katika kufanya maamuzi binafsi katika kupanga bei za internet bila ya kumuangalia mtumiaji wa mwisho
ambae ni Mtanzania Masikini.
Napata ugumu kuamini Tanzania inayotafuta maendeleo kwenye nyanja hii kwanini iweze kukubali na kuwaachia makampuni ya simu kufanya Price Fixing watakavyo huku wakishusha
viwango vya internet (MB) na kuongeza thamani ya gharama kwa watumiaji wa Tanzania ambao ni masikini huku wizara husika ipo, Competition Commission, Competition And
Consumer Protection Policies zipo na wahusika wapo wanafumbia macho tu.
Tukitaka Tanzania iendane na dunia inavyokwenda na kuongezeka kimaendeleo katika nyanja hii na tukitaka kwenda sambamba na Mtazamo madhubuti na ulio mzuri wa Mheshimiwa
Rais wetu Magufuli wa kuiletea Tanzania maendeleo kwenye kila nyanja na kutaka kufanya Tanzania liwe Taifa lenye nguvu duniani na lenye watu walio elimika ni vyema wahusika wakahakikisha haya makampuni ya simu hayafanyi Price Fixing maana ukiangalia
kwa undani viwango vyao vya kuuza internet vyote vimepangwa sawa sawa na vyote wamevishusha kwa wakati mmoja bila ya kutoa sababu ya msingi inayo wafanya kuongeza gharama
na kushusha viwango vya internet wakati Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umepita Tanzania.
Wahusika kama mkishindwa kuwatetea Watanzania walio wanyonge, Mheshimiwa Rais Magufuli hili ni jipu tunaomba uanze kutumbua kwenye sekta hii ya mawasiliano.
Ni matumaini yetu wahusika na wadau wote watakutana na kuweza kulitafutia mchakato madhubuti kwa kuwatetea watumiaji wa simu na internet nchini Tanzania na vile ili
kuweza kuleta maendeleo nchi nzima na kuwawezesha ata Mtanzania aliyepo Chato au Sumbawanga aweze kupata fursa ya kuunganishwa na dunia kwa kupata viwango vya bei
iliyo nzuri na viwango vikubwa vya internet.
Vile vile kuanzia sasa haya makampuni ya simu kamwe yasifumbiwe macho kwa bei wanazozipanga kwenye huduma ya mawasiliano kwa maana yanawanyonya Watanzania ambao ni masikini kwa manufaa yao!
Vile vile kuanzia sasa haya makampuni ya simu kamwe yasifumbiwe macho kwa bei wanazozipanga kwenye huduma ya mawasiliano kwa maana yanawanyonya Watanzania ambao ni masikini kwa manufaa yao!
No comments:
Post a Comment