
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akipungia mkono vikundi vya utamaduni vilivyokuwa vikitoa buradani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kabla ya
kuondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili
nchini.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiagana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya kuondoka jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akishukuru kabla ya kuondoka baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wafanyakazi wa kitengo cha mizigo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JINIA jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment