
Magdalena Mosha akiwa pamoja na mshiriki mwenzie Hilal Hilal wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya kuondoka kuelekea nchini Brazil.
Na Zainab Nyamka.
WAWAKILISHI
wa Tanzania katika michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika katika
mji wa Sao Paulo, Rio De Jeneiro nchini Brazil , timu ya kuogelea
imefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya kukabidhiwa bendera na Kamati
ya Olimpiki nchini TOC kwa ajili ya kuiwakilisha vyema katika mashindano
hayo.
Timu
hiyo itakayowakilishwa na waogeleaji wawili ambao ni Magdalena Moshi
anayeenda kwa mara ya tatu kwa upande wa wanawake huku Hilal Hilal
akienda kwa mara ya kwanza na wote watakuwa ni waogeleaji katika upande
wa mita 50. Akizungumzia maandalizi ya mwisho Kocha wa timu hiyo
Alexandra Mwaipasi amesema kuwa wachezaji wake wameiva kwani mwanzoni
walikuwa na changamoto ya kupata mabwawa yenye viwango vinavyoendana na
mashindano hayo ila kwa mwaka huu washiriki wote wameweza kuweka kambi
katika nchi mbili tofauti ambapo Magdalena amekuwa Australia huku Hilal
akijifua nchini Dubai.
Amesema,
ana imani na wachezaji wake kwani kwa kipindi alichokaa nao ameona
uwezo waliokuwa nao na wanaweza kurudi na medal nyumbani. Naye Katibu
mkuu wa chama cha kuogelea TSA Ramadhan Namkoveka amesema kuwa tofauti
na wengine wao hawajapata wadhamini ila wachezaji wao wamejiandaa vizuri
na wana imani kubwa kuwa wataweka historia.
Moja
ya washiriki, Magdalena Mosha amesema kuwa amejiandaa vizuri na
anaamini miaka aliyoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing na
London yamempa uelewa zaidi wa nini anatakiwa kufanya mwaka huu na
katika mazoezi yake nchini Australia ameyafanyia kazi. Amesema kuwa kwa
sasa macho ya watanzania yapo kwao na wanatoa ahadi ya kufanya vizuri
kwani hata mshiriki mwenzie Hilal amekuwa kwenye mazoezi mazuri nchini
Dubai tena katika kituo kinachojihusisha na masuala ya uogeleaji.
Timu hiyo kesho inakabidhiwa bendera na TOC kabla ya Agosti 02 kuondoka kuelekea nchini Brazili.
Magdalena na Hilal wakiwa katika mazoezi ya mwisho.
Viongozi wa Chama cha Kuogelea TSA wakiwa pamoja na washiriki Hilal Hilal na Magdalena Mosha, Kushoto ni mkurugenzi wa ufundi Amina Mfaume, Mwenyekiti wa TSA Alex Mosha, Katikati ni Kocha wa timu ya kuogelea Alexandra Mwaipasi na mwisho kulia ni Katibu mkuu TSA Ramadhan Namkoveka.




No comments:
Post a Comment