HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 11, 2016

TRACTO Co. Ltd WASHIRIKI MAONYESHO YA AUTO EXPO - MLIMANI CITY

Kampuni ya Tracto Co Ltd ni Wasambazaji rasmi wa Cummins Filtration ( Fleetguard ) na vilainishi vya Magari na Mitambo aina ya Valvoline nchini Tanzania.

Dhamira ni usambazaji wa bidhaa bora ili kuruhusu wasimamizi na wamiliki wa magari na mitambo kupunguza gharama za uendeshaji huku wakizingatia ubora. Timu ya wataalamu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Cummins na Valvoline hufanya kazi bega kwa bega na watumiaji wa mwisho wa bidhaa hizo kuhakikisha wanaitumia bidhaa kwa ufasaha na kuepuka majanga yatokanayo na utumiaji wa bidhaa hafifu. Utendaji umejengwa juu ya nguzo 4 ambazo ni:

Uchujaji/Filtration - Kuondoa Uchafu kutumia Bidhaa bora duniani kama - Fleetguard , MANN na PALL.

Vilainishi/Lubricants – Kampuni ya Tracto Co Ltd wanasambaza vilainishi bora kutoka Valvoline na Lubrication Engineers. Hivi ni vilainishi visivyokuwa na uchakachuaji wowote, wanakupa ubora uleule ulio pendekezwa na wazalishaji wa vyombo vyote vya moto.

Uhifadhi wa Mafuta – Hii hufanyika kwa kutumia matanki imara kabisa yaliyojengwa kwa kuta mbili, na huwekwa juu ya aridhi hivyo kurahisisha usafishaji na pia kurahisisha usafirishaji iwapo unataka kuhama, vivyo hivyo kuweza kugundua itilafu yoyote ikitokea katika tanki.

Uchunguzi na ufuatiliaji – Tunafanya Uchunguzi na Ukaguzi wa Mafuta kuona kiwango cha Usafi wake, na Kutoa ushauri kuhusu nini unatakiwa kukifanya kama mafuta yako tayari yana uchafu.
Afisa Mkuu wa Masoko ndg. Victor Ndamugoba akielezea bidhaa zao kwa watu waliofika kwenye banda lao (hawapo pichani).
Watu waliopata nafasi kutembelea banda la Tracto wakipata maelezo kutoka kwa wataalam kutoka Tracto.
Martin (mwenye nguo nyekundu) mtaalam wa vilainishi kutoka Valvoline akisiliza swali kwa makini kutoka kwa mmoja wa mteja aliyepita kutembelea banda la Tracto.
Mkurugenzi Mkuu Wa Tracto Ndg. Luk akielezea wageni aina mpya ya tanki la kuhifadhia mafuta kama bile Petrol, Dieziel nk. ambayo imetengenezwa na Tracto hapa hapa Tanzania.
Kikosi kazi kutoka Tracto wakiwa kwenye picha ya pamoja.

1 comment:

  1. wow great,nowadays this type of blog is more important and informative technology,it was more impressive to read ,which helps to design more in effective ways


    salesforce Training instiute in Chennai

    ReplyDelete

Post Bottom Ad