Thursday, July 21, 2016

TIMU YA VIJANA IPO MBIONI KUKAMILIKA-YANGA.

Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kupata kikosi cha timu B cha vijana wa chini ya miaka 20 kwani kwa sasa wameshateua wachezaji na wanatarajia kumfanya mchujo kamili ili kuunda kikosi hicho.

Maboresho hayo yanafanywa kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho cha vijana na hasa baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF kuanzisha ligi ya vijana Kwa timi zote zinazoshiriki ligi kuu na itakwenda sambamba na ratiba ya ligi kuu Vodacom itakayoanza Agosti 20 mwaka huu.

Deusdedit amesema kuwa kwa sasa Kocha wa vijana anaendelea na programu yake kama kawaida na atakapokuwa tayari atatoa tathmini yake juu ya wachezaji wote na kisha kufanya mchujo wa mwisho na kisha kuendelea na na mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo ya vijana.

"Kwa sasa kocha anaendelea na kazi ya kuwaangalia wachezaji waliopita mchujo wa kwanza, programu imaendelea katika uwanja wa Kaunda na itakapokuwa tayari mwalimu ataweka wazi wachezaji watakaoonesha kiwango kizuri na kuanza mazoezi rasmi ya ligi ya vijana,"amesema Deusdesit.

Wakati huo, Deusdedit amesema kuwa uongozi wa Yanga hauna taarifa zozote juu ya mkataba wa kurusha haki za matangazo kwa kampuni ya Azam kuwa wao hawana taarifa hizo na wala hawakuhusishwa wakati wa makubaliano yoyote. Kwa sasa tupo kwenye mikakati ya kujadiliana na tutaoa tamko letu juu ya mkataba huo na zaidi tutaongelea suala la kutokuchukua fedha zile za awali.

No comments:

Post a Comment