Thursday, July 21, 2016

MIMBA ZA UTOTONI ZIMEONGEZEKA WASTANI WA ASILIMIA NNE.

Wadau wa masula ya watoto wakisikiliza maada katika mkutano wa kujadili ndoa za utotoni katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Watetezi haki za watoto wakiwa katika picha ya pamoja baada katika mkutano wa kujadili juu ya kutaka sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurgenzi wa Shirila Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti akichangia maada katika mkutano wa kujadili ndoa za utotoni katika mkutano wadau wa masuala ya watoto uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TAKWIMU zinaonyesha kwamba mimba za utotoni zimeongezeka kwa wastani wa asilimia nne kutoka asilimia 23 mwaka 2010,hadi kufikia asilimia 27,mwaka Jana kutokana na kukosa uwekezaji kwa watoto wa kike.

Akizungumza kwenye mkutano wa Nijali Media Dialogue ulioandaliwa na Shirika la C-SEMA, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja Wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA),Christina Kwayu, amesema wasichana wenye umri chini ya miaka  18 wamekuwa wakiolewa kwa idadi kubwa.

Amesema ndoa hizo zinasababisha  kuwepo kwa mimba za utotoni na ndio nas kufanya wadau wa masuala ya watoto kupigia kelele juu ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe ili kuweza msichana kutimiza malengo yake.

"Japo baadhi ya imani ya dini zinasema mtoto chini ya miwote aka 18 anaweza kuolewa lakini haijatoa nafasi ya kumlazimisha msichana kuolewa",amesema Kwayu.

Naye Mkurugenzi Wa Shirika la Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti, amesema kati ya watoto watano,watoto wawili wanaolewa hapa nchini.

Amsema hukumu iliyoyolewa na mahakama kuu kuhusu umri wa mtu kuolewa kuwa ni miaka 18, itumiwe kama sehemu ya kuwashitaki wale wote wanaooa watoto.

Mtengeti, mchakato wa kubadilisha sheria ya ndoa umefika katika hatua nzuri na kuwataka wadau wote kuwa na nguvu ya pamoja katika kumtetea msichana waTanzania.

Amesema utekelezaji wa hilo litafanikiwa pale wadau wataposhinikiza wabunge kubadilisha sheria hiyo na kuwataka watunge Sera na sheria walichukue hilo na kulifanyia kazi.

Kwa upande wake,Afisa Jinsia kutoka Shirika la Kimataifa  la Vijiji vya Watoto(SOs), Catherine Kasimbazi, alisema kubadilishwa kwa vipengele ambavyo vina mkandamiza mtoto ni hatua nzuri katika msichana kuweza kupata utu wake.

Amesema dhamira ya Nijali ni kuwajali watoto na kwamba sheria ya ndoa ikibadilishwa usawa kati ya mtoto wa kike na wakiume utakuwepo.

Mkutano huo ulioandaliwa na Csema kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Australia uliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za watoto.

No comments:

Post a Comment