NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amefanya uzinduzi rasmi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), uliofanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa Seashells Millenium Hotel, Jijini Dar es salaam
Shirika hilo lililoanzashwa na Mwanafuzi wa fani ya Udaktari, Juliana Busasi limefanikiwa kufikisha huduma zake za afya na elimu ya afya kwa watanzania Zaidi ya 1327, likiwa na Dira ya Kuboresha Afya na Ustawi Nchini na kuweka mikakati imara kwa ajili ya Kuboresha afya Tanzania katika Nyanja kuu tatu ambazo ni Kuongeza Ubora wa Huduma za Afya zinazotolewa Nchini, Kueneza elimu juu ya kupambana na changamoto mbalimbali za Afya, Kuboresha mipango mikakati ya Kujikinga na magonjwa ambukizi na yasiyo ambukizi kupitia program ya mpya iitwayo NURU YA AFYA.
Dkt. Kigwangalla aliunga mkono jitihada hizo za TAHMEF na kwa kutambua uhumimu wa jambo hilo, alichangisha fedha kwa ajili ya Kutoa msingi mzuri kwa shirika hilo ili kufanikisha Juhudi za Kuboresha Taifa katika Nyanja za Afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimpongeza Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi kwa jitihada anazofanya za kusaidia jamii katika nyanja ya Afya na Tiba.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akihutubia katika Uzinduzi huo.
Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi akizungumza.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na baadi ya washiriri na viongozi wa Shirika hilo.
No comments:
Post a Comment