HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 10, 2016

DAR JOGGING WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA VIONGOZI KULETA MAENDELEO

Na Zainab Nyamka

KIKUNDI cha Dar Jogging kimetakiwa kutumia vizuri fedha walizozipata kwa kuanzisha miradi itakayowaletea maendeleo na kuinua zaidi kikundi chao ikiwemo kufika mbali zaidi kiuchumi na kutumia fursa ya viongozi wa siasa waliokuwa nao kuweza kuwawezesha na sio kusubiri wao wawatumie kwa manufaa hayo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho ambaye pia ni katibu mkuu wa chama  cha kuogelea nchini TSA Ramadhan Namkoveka amesema kuwa wamefurahi sana kuona vijana wanaungana na kutengeneza umoja ambao utakuja kuwa na mlengo wa maendeleo na hasa kwa hatua waliyofikia ya kuungana na vikundi nane kutoka maeneo mbalimbali ikijumlisha wilaya ya Temeke na Kinondoni na kuanzisha mchezo wa upatu.
 Mbunge wa jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea amewataka wanavikundi vya Jogging kuwatumia ili kutengeneza fursa za ajira na kuweza kuinua vipato vyao ikiwemo kuanzisha miradi mbalimbali itakayokuwa na manufaa kwao na kuacha kutumiwa na wanasiasa hususani wakati wa kampeni unapofika. Hayo amesema leo katika viwanja vya shule ya Mabatini mbio zilipoishia ikiwa ni katika kuendeleza fursa waliyoipata takribani vikundi nane vilivyoamua kujiunga na kuanzisha mfuko wa kupeana ujulikanao kama upatu.

Akizungumza na vikundi hivyo, Mtolea amesema kuwa mchango mkubwa wa maendeleo unaletwa na vijana na kama watashindwa kutumia nafasi ya miaka mitano kwa viongozi wao basi bila shaka watatumiwa wao katika kipindi cha kampeni. "Nawataka vikundi vyote viweze kututumia sisi wanasiasa katika kuleta maendeleo na katu msikubali kutumiwa kwani mtakapopata nafasi ya kuanzisha miradi mbalimbali itakuwa ni mafanikio makubwa sana kwa taifa letu hususani kwenye kuinua uchumi pamoja na sekta ya ajira kutanuka zaidi na kupunguza upungufu wa vijana kukaa bila kazi,"

Vikundi vilivyoungana na kutengenza umoja huo  ni Dar Jogging, Temeke Family, Dovya Jogging, Wasafi Jogging, Tupo Jogging, Ferry Jogging kutoka wilaya ya Temeke, Mzimuni Jogging na Barafu Jogging kutoka Magomeni wilaya ya Kinondoni na utaratibu wao ukiwa ni kila kikundi kuwasilisha laki moja (100,000) kila mwisho wa mwezi na kimoja wapo kupatiwa fedha taslimu laki nane. (800,000)
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (kati) akijumuika na wanajogging wengine kufanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza mbio zilizoanzia Uwanja wa Taifa mpaka Uwanja wa shule ya Mabatini, Tandika magorofani
Wanajogging wafanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza mbio zilizoanzia Uwanja wa Taifa mpaka Uwanja wa shule ya Mabatini, Tandika magorofani.
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (kati) akizungumza na wanajogging mara baada ya kukabidhi fedha taslimu kiasi cha laki nane (800,000) kwa mweka hazina wa Dar Jogging Mariamu Mkama (kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Dar Jogging Ramadhan Namkoveka (kushoto)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad