Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na Mji wa Kibaha mkoani pwani kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 72, kuanzia siku ya Ijumaa 17/06/2016, Jumamosi 18/06/2016 na Jumapili 19/01/2016.
Sababu ya kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Juu ni kumruhusu Mkandarasi (WABAG) kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani. Kazi hii ikikamilika, uzalishaji unategemea kuanza mara moja, hivyo kumtua mama wa Dar es salaam ndoo Kichwani.
Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo yafuatayo kukosa Maji:
MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, KIBANGU, MAKUBURI PAMOJA NA ENEO LOTE LA TABATA, SEGEREA HADI KINYEREZI.
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA
DAWASCO INAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
No comments:
Post a Comment