MKUU WA Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka watu wa china kuwekeza katika jiji la dar es salaam kutokana mji huu kuwa kitovu cha biashara nchini.
Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa biashara wa kirafiki kati ya jimbo la Jiangsu la nchini China na mkoa wa Dar es salaam, Makonda amesema kuwa ushirikiano wa kirafiki kati miji hiyo miwili utatatua baadhi ya changamoto zilizopo katika jiji la dar es salaam na taifa kwa ujumla
Makonda amesema kuwa watu wa china wana uzoefu kutokana kupiga hatua za kiuchumi hivyo Dar es salaam itaweza kupanda kiuchumi kutokana na mazingira yaliyowekwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (pili kulia) akibadilishana nyaraka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Jimbo la Jiangsu nchini China, Luo Zhijun mara baada ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara wa kirafiki kati ya Jimbo hilo na Jiji la Dar es salaam, leo Juni 3, 2015. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Jimbo la Jiangsu nchini China, Luo Zhijun wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara wa kirafiki kati ya Jimbo la Jiangsu na Jiji la Dar es salaam, leo Juni 3, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara wa kirafiki kati ya Jimbo hilo na Jiji la Dar es salaam, leo Juni 3, 2015.
Baadhi ya Wadau waliohudhulia hafla hiyo.





No comments:
Post a Comment