HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 15, 2016

RAIS MAGUFULI AANDAA FUTARI YA PAMOJA YA VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika foleni na wageni wake kwenda kuchukua chakula wakati wa kufuturu katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipongezwa na kaimu Mufti Sheikh Hamid Masoud Jongo baada ya kuongea machache katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' na wagemi wengine wakipakua chakula katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad