Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB), Devota Mdachi (kulia) akimkabidhi Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16), Aeesha Kamara, kitabu maalum kinachoelezea sifa kem kem za Tanzania, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia Watanzania mbalimbali waishio ndani na nje ya nchi. Mbali na Mrembo huyo, Bodi ya Utalii, ilikutana pia na Mchezaji wa mpira wa Miguu wa kimataifa, Mbwana Samatta pamoja na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini, Vanessa Mdee.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB), Devota Mdachi (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa, Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16), Aeesha Kamara, mara baada ya kuzungumza nae leo.

Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16), Aeesha Kamara akifafanua jambo, wakati alipokutana na Bodi ya Taifa ya Utalii, jijini Dar es salaam leo.
Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16), Aeesha Kamara (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB), mara baada ya kufika na kuzungumza na Bodi hiyo, leo Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mama mzazi wa Mrembo huyo,
No comments:
Post a Comment