HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2016

TFF IMESEMA ILIKUA HALALI AZAM KUPOKWA POINTI 3 KUFUATIA KUMCHEZESHA ERASTO NYONI.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUFUATIA kunyang'angwa kwa ponti 3 za Azam walipocheza dhidi ya Mbeya City,  Azam kulalamika wakihitaji kupata mrejeo wa adhabu hiyo hatimaye kamati ya masaa 72 imetoa majibu yake baada ya kukutana.

 Azam walituma barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wakilalamikia maamuzi yaliyotolewa na Bodi ya Ligi ya kunyang'anywa alama zao 3 muhimu kufuatia kumchezesha Erasto Nyoni katika mechi yao dhidi ya Mbeya City.

Akitoa ufafanuzi baada ya kukutana kwa kamati hiyo, Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo wakaamua kukaa chini tena na kuangalia upya ripoti zote za waamuzi na kugundua hakuna uonevu uliofanyika.

"Kamati ya masaa 72 imekaa pamoja  na kupitia ripoti zote za waamuzi wa mechi alizocheza Azam na kugundua kuwa hakuna sehemu wamekosea au kufanya uonevu dhidi ya Azam,"amesema Lucas. Mrejeo huo umekuja baada ya Azam kutuma maombi yao kwa TFF ya kurejea ripoti zote za waamuzi wa michezo yao na baada ya kukaa kamati wamegundua kuwa walikuwa sahihi katika maamuzi ya awali.

"Tumejidhihirisha kabisa kuwa Nyoni amecheza akiwa na kadi  3 za njano alizozipata kwenye mechi tatu tofauti akiwa na timu yake ya Azam,"amesema Lucas.

Kamati imepitia mechi zote za Azam na kugundua katika mchezo wa Ngao ya Jamii Nyoni alipata kadi ya Njano pamoja na mchezo wa Prison na wa Coastal Union ambapo kulingana na kanuni ya  37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake hivyo Azam wamekwenda kinyume na Kanuni husika, uzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi 3 na mabao matatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad