HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2016

TAKUKURU KUELIMISHA JAMII NA KAMPENI YA 'LONGA NASI'.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA.

UZINDUZI WA KAMPENI YA KUELIMISHA UMMA YA
 ‘LONGA NASI’ MEI 24, 2016.
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), katika kutekeleza jukumu la ‘kushirikisha umma katika mapambano dhidi ya rushwa’, imeandaa kampeni ya kuelimisha umma iliyopewa jina la LONGA NASI. 

Kampeni hii itatumika pia kuitangaza huduma mpya ya kutoa taarifa za rushwa kwa kupiga *113# au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kwenda namba 113 kutoa maoni, taarifa au kuuliza maswali kupitia mitandao ya AIRTEL, HALOTEL, TIGO, VODACOM na ZANTEL. Huduma hii ya bure kwa wananchi itazinduliwa rasmi wakati wa uzinduzi wa kampeni tajwa.

Uzinduzi huu unatarajiwa kufanyika Jumanne - Mei 24, 2016 katika uwanja wa Mwembeyanga, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kuzinduliwa, kampeni hii itafanyika nchi nzima na kushirikisha makundi yote ya jamii.

WANANCHI WOTE WANAKARIBISHWA KUHUDHURIA KATIKA KAMPENI HII.
Imetolewa na Ofisi ya Afisa Uhusiano, TAKUKURU Makao Makuu, Mei 20, 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad