HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2016

MGAMBO WAJIZATITI DHIDI YA AZAM.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
 TIMU ya Mgambo JKT(Pichani) imesema kuwa itapambana kufa na kupona katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Azam FC kuhakikisha wanasalia ndani ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao. Timu hiyo iliyo katika hatari ya kushuka daraja imevuna pointi 27 katika michezo 29 waliyoicheza. 

Kati ya michezo hiyo 29 Mgambo amefanikiwa kushinda mechi tano, ametoa sare katika mechi tisa huku akipoteza michezo 15. Kocha Mkuu wa timu hiyo Joseph Lazaro amesema  kuwa mchezo huo kwao ni kama fainali hivyo watahakikisha haupotezi.

Amesema kuwa licha ya michezo mingi ya ugenini kuwa migumu lakini kwao hauwezi kuwa changamoto kutokana na maandalizi wanayoyafanya kuelekea mchezo huo huku akiwa  anaimani kubwa na wachezaji wake katika mchezo huo kwani lengo la kila mmoja ndani ya kikosi chao ni kuinusuru timu hiyo kutoangukia katika balaa la kushuka daraja. 

"Wachezaji wangu wanaelewa kuwa mchezo huo ni mwamuzi wa mwisho utakaoamua aidha timu yetu kusalia ndani ya ligi au ndo utakuwa mwisho wetu", amesema Lazaro. Endapo timu hiyo itashindwa kuizamisha Azam katika uwanja wao wa nyumbani basi ndo itakuwa tiketi yao kuelekea ligi daraja la kwanza msimu ujao. Lakini endapo watashinda mchezo huo kazi kubwa itakuwa ni ziombea mabaya timu za Kagera Sugar na JKT Ruvu ambazo wamepishana nazo kwa pointi chache.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad