HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2016

MASHINDANO YA KIKAPU KANDA YA TANO KUFANYIKA JULAI 19.

Na Zainab Nyamka, Mtaa kwa Mtaa
MASHINDANO ya Afrika kanda ya tano ya mpira wa Kikapu amesogezwa mbele hadi Julai 19 kutokana na kukosa fedha za kuandaa mashindano hayo kwa sasa hadi pale bajeti ya serikali itakapopitisha mwaka mpya wa kifedha.

Mwenyekiti wa mashindano  na katibu mkuu msaidizi Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini  (BFT) Mwenze Kabinda amesema wamepokea taarifa hizo ila awali timu zimeshaanza kujiandaa kwa ajili ya michuano hyo ya kanda ya tano Afrika.

"Tumepokea barua kutoka kwa katibu mkuu wa Kanda ya tano Afrika kutoka nchini Misri akisena kuwa michuano hiyo itasogea mbele hadi julai 19 na kumalizika Julai 24,"amesema Kabinda.

Mashindano hayo yanakuwa ni kwa nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Egypt, Eritrea, Ethiopia, Somalia Rwanda, Sudani na Sudan kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad