HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2016

GOLIKIPA WA TIMU YA PRISONS APANIA TIMU YA TAIFA.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
GOLIKIPA wa timu ya Prisons, Beno Kakolanya amefurahi kuweza kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa na amesema atahakikisha Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa hajutii maamuzi yake ya kumuita ndani ya kikosi chake. 

Hii ni mara ya kwanza kwa golikipa huyo wa kutumainiwa ndani ya kikosi cha Prisons kuitwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa lakini Msimu uliopita Beno hakupata nafasi ndani ya kikosi chake huku akifanikiwa kudaka mechi tatu na toka alipoanza kucheza mpira malengo yake makubwa yalikuwa ni kujituma ili siku moja ndoto zake zije kutimia.

Amesema, kwa sasa amepata nafasi hiyo atahakikisha anaitumia vema hasa katika maandalizi ili kupata nafasi ya kudaka katika mechi mbili zilizo mbele yao. "Nitahakikisha Mwalimu Mkwasa hajutii maamuzi yake ya kunijumuisha ndani ya kikosi chake na nitajitahi kufanya vizuri katika mandalizi ya michezo yetu miwili ule wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars ya Kenya pamoja na ule wa AFCON dhidi ya Misri", amesema Beno. 

Beno ameanza kupata nafasi ndani ya Prisons msimu wa Ligi wa 2013/14 baada ya aliyekuwa golikipa namba moja wa timu hiyo kuvunjika kidole huku golikipa namba mbili akipumzishwa baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo. Msimu wa Ligi wa 2014/15 golikipa huyo alicheza mechi tatu huku msimu huu akizikosa mechi takribani 10 za awali kutokana na maumivu ya bega yaliyomuweka nje kwa miezi miwili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad