HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2016

DROO YA MAKUNDI YA CAF MEI 24.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BAADA ya kumalizika kwa hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho na kufanikiwa kupatikana kwa timu 8 zilizoingia kwenye makundi hatimaye Droo ya kupanga timu hizo inafanyika Jumanne ya Mei 24.

Shirikisho la mpira wa miguu Aftika (CAF) limeamua kupanga ratiba hiyo na hatua ya makundi itaanza kupigwa Juni 17.

Wajumbe wa kamati ya Mashindano watakutana Jumatatu Jijini Cairo nchini Misri makao makuu ya CAF  ili kuweza kufanya mchakato wa kuandaa taratibu za kupanga makundi katika timu 8  ili kuweza kujua timu gani zinakaa pamoja.

Timu zilizofanikiwa kuingia Young African (Tanzania) , TP Mazembe ( DRC) , Etoile Du Sahel ( Tunisia),
3 Mo Bejaia (Algeria), Madeama (Ghana), Kawkab Marrakech (Morocco), Al Ahly Tripoli (Libya) ,Fus Rabat (Morocco).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad