Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. Meron, Rais wa MICT.
Picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals- (MICT), Mhe. Dkt.Serge Bremmertz. Katika mazungumzo yao Mwendesha Mashtaka huyo aliipongeza Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuridhia taasisi za Umoja wa Mataifa zinazosimamia sheria kujengwa nchini na kuielezea Arusha kama makao makuu ya kimataifa ya haki kwa Ukanda wa Afrika. Pia aliahidi ushirikiano hususan katika kuwajengea uwezo wataalam wa masuala ya sheria za kimataifa hapa nchini.
Sehemeu ya Wajumbe waliofuatana na Mwendesha Mashtaka wa MICT.
Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Mwendesha Mashtaka wa MICT, Dkt. Bremmertz. Picha na Reginald Philip

No comments:
Post a Comment