HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 19, 2016

UJUMBE WA JWTZ WAKUTANA NA BALOZI HAULE.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, ametembelewa na Viongozi wa ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Dar es Salaam, ambao uko nchini Kenya kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja. Ujumbe huo unaongozwa na Kamanda wa Chuo cha Ulinzi, Meja Jenerali Yacoub Mohamed, na unajumuisha Maafisa na Washiriki wa Kozi 12.
Makundi mengine matatu kutoka chuo hicho kilichoko Kunduchi yako kwenye ziara kama hii nchini Afrika Kusini, Botswana na Namibia.
Picha ya Pamoja, Luteni Kanali Maulid Surumbu, Bw. Johnson Nyingi, Mwakilishi wa Jeshi la Kenya, Kanali Sebestian Likaunye, Meja Jenerali Mohamed, Balozi Haule, Luteni Kanali Machemba na Kamishina Msaidizi wa Magereza Phaustine Kasike.
 Balozi Haule (kulia) katika mazungumzo na Vingozi waliomtembelea. Wapili kulia ni Meja Jenerali Mohamed na Kushoto ni Mwambata wa Kijeshi Ubalozini, Luteni Kanali Fabian Machemba.
 Meja Jenerali Mohamed akimkabidhi Balozi Jarida lililochapishwa na Chuo cha Ulinzi kwa heshima ya Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad