Kuelekea siku ya Malaria Duniani ambayo kitaifa huadhimshwa tarehe 25 Aprili, Shirika la Afya na Elimu
ya Tiba (TAHMEF) limetoa huduma ya upimaji wa Afya tarehe 23 Aprili katika msikiti wa Masjid Al Ghadir, uliopo Kigogo, Jijini Dar es salaam.
Huduma hiyo ilihusisha upimaji wa Malaria, kisukari, shinikizo la damu na upungufu wa damu, ambapo Matibabu ya
Dawa na ushauri ulitolewa kwa wananchi waliobainika kuwa maradhi hayo, chini ya uangalizi wa madaktari
wazoefu.
Jumla ya wananchi 352 walipata huduma hii, wanawake wakiwa 150 na wanaume 202 kati ya idadi hiyo.




No comments:
Post a Comment