Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation) yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili kujiinua kiuchumi hasa Mama Lishe kwa kushirikiana na wadau mbali mbali. Uzinduzi huo umefakika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Basila Mwanukuzi (kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja pamoja na Mwakilishi wa Mama Lishe, Bi. Grace Foya.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu,
akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi
(Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation), uliofanyika kwenye Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2016.

Mwanzilishi
wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment
Foundation), Basila Manukuzi, akizungumza machache wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Taasisi yake hiyo yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua
uwezo wao wa kibunifu ili kujiinua kiuchumi hasa Mama Lishe uliofakika
leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es
salaam
Familia ya Basila Mwanukuzi, wakifatilia hafla hiyo.

Baadhi ya wageni waalikwa kutoma sehemu mbali mbali.
Baadhi ya wakina Mama Lishe kutoka Wilaya za Ilala na Kinondoni wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wadau.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu, akisalimiana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao
ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania, Anko Hashim Lundenga wakati
walipokutana kwenye hafla hiyo.

Picha ya pamoja na baadhi wa Wageni wa waalikwa pamoja na Kina Mama Lishe.









No comments:
Post a Comment