(Picha zote na Andrew Chale.)
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.
Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.
Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.
No comments:
Post a Comment