HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 8, 2016

KESI YA BOSS WA ZAMANI WA TRA YASIKILIZWA TENA LEO

Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo, mara baada ya kusikilizwa kwa kesi inayowakabili yeye na wenzake wawili ambao ni waliokuwa Maafisa Waandamizi wa Benki ya Stanibic Tanzania, Shose Sinare pamoja na Sioi Solomoni waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa makosa manane likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani.

Kesi hiyo imesikilizwa tena leo Mahakamani hapo, ambapo baada ya kusikilizwa kwa muda wa takribani masaa matatu, kesi hiyo imeahirishwa mpaka Aprili 22 itakapotajwa tena na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani, Shose Sinare akisindikizwa na Askari wa Jeshi la Magereza kwenda kwenye gari maalum, tayari kwa safari ya kurudishwa rumande baada ya kesho yao kusogezwa mbele.
Sioi Solomoni akijiangaa kupanga Gari hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad