Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.
Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua Rais. Majina yao ndiyo haya:
1 Khamis Iddi Lila ACT-W
2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA
3 Hamad Rashid Mohamed ADC
4 Said Soud Said AFP
5 Ali Khatib Ali CCK
6 Ali Mohamed Shein CCM
7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA
8 Seif Sharif Hamad CUF
9 Taibu Mussa Juma DM
10 Abdalla Kombo Khamis DP
11 Kassim Bakar Aly JAHAZI
12 Seif Ali Iddi NRA
13 Issa Mohammed Zonga SAU
14 Hafidh Hassan Suleiman TLP

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha alipokuwa akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa marudio jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,ambapo Mgombe wa Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein kaibuka kushinda uchaguzi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akipokea cheti maalum cha Ushindi wa Uchaguzi wa marudio kutoka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akionesha Cheti maalum cha Ushindi baada ya kukabidhiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akisalimiana na Wagombea wa Vyama vya Siasa baada ya kutangazwa mshindi jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ADC Bw,Hamad Rashid baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa Cheti rasmi cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia
CCM na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakishangilia kwa makofi wakati
alipotangazwa kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
Jecha Salim Jecha jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia
CCM na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipongezwa na Mgombea wa Urais
kupitia Chama cha ACT-Wazalendo Bw,Khamis Iddi Lila (wa pili kulia)
baada ya kutangazwa mshindi wakati matokeo ya uchaguzi huo jana katika
ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia
CCM akipongezwa na Watoto wake baada ya kutangazwa mshindi wakati wa
matokeo ya uchaguzi huo jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini
Unguja.

Mgombea
wa Urais kupitia Chama cha ADC Bw,Hamad Rashid Mohammed akitoa
shukurani kwa niaba ya Vyama mbali mbali vilivyoshiriki uchaguzi wa
marudio baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa Cheti rasmi cha
ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha
jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akipongezwa na Mgombea wa Urais kupitia Chama cha AFP Said Soud Said baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa Cheti rasmi cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapindiuzi (CCM) na Wananchi na Vyma vya Upinzani waliohudhuria katika hafla ya utolewaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Marudio katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja jana.
Viongozi mbali mbali wa CCM na vyama vya upinzani wakishuhudia matokeo ya uchaguzi Mkuu wa marudio yaliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Viongozi mbali mbali wa vyama vya upinzani wakishuhudia matokeo ya uchaguzi Mkuu wa marudio yaliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,ambapo mshindi ametangazwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM.










No comments:
Post a Comment