Huduma ya usafiri wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani
miezi miwili sasa imerejea kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa reli
hiyo katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema
hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo
ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni
mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko
vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam kwenda bara itapita na
kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi
wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara,
Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na
mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli
bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi
ya reli.
Amesema Shirika la Reli Tanzania ( TRL)
linaendelea kuhakikisha kuwa treni inayopita kwenye reli ya Kati
inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga na Dar Es
Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara
watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya
barabara.
Waziri Profesa Mbarawa ameteembelea bwawa la
Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa
mvua za Vuli na Masika katika mikoa ya Dodoma na Iringa.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa John Henjewele amemhakikishia Waziri Profesa
Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi
wanaoishi karibu na reli ya Kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka
wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.
Takribani
Shilingi millions 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia
uharibifu uliotokea mwezi Januari na kukata Mawasiliano ya reli Kati
ya mikoa ya Dodoma na Morogoro na kusababisha Safari za treni kutoka
bara kuishia Dodoma.
Treni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa
ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati
ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa
Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Felix Nlalio, kuhusu namna ya kudhibiti mkondo
wa maji katika mto mkondoa yasiathiri hifadhi ya reli.
Muonekano wa Sehemu ya Reli katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya ukarabati kufuatia
mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa
Morogoro na Dodoma.
Kazi za ukarabati wa mwisho zikiendelea katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya ukarabati
kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya
Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa viongozi wa
Shirika la Reli Tanzania (TRL), kuhusu namna ya kushirikisha wananchi kulinda hifadhi ya reli.

No comments:
Post a Comment