Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Kamishna wa
Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari Sururu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimuuliza jambo Kamishna
wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa
na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya
Jeshi hilo, mjini Magharibi Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na
Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi,
Wakuu wa Upelelezi pamoja na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Kulia meza
kuu ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akipewa maelezo na
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame (kulia) wakati wa kikao chake na
Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi,
Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:
Post a Comment