Na Mwandishi Wetu,Arusha
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dr.Frida Mokiti
amewashauri wakazi wa jiji la Arusha kujiunga na Bima ya
Afya ya Resolution Insurance katika uzinduzi wa Tawi
jipya lililofanyika mwishoni mwa wiki katika jengo la NSSF
– Mafao House na baadae chakula cha jioni katika Hoteli
ya Maunt meru.
Dr. Frida aliipongeza Kampuni ya Resolution
Insurance kwa kufungua tawi jipya jijini Arusha ikiwa ni
sehemu ya kuwasogezea huduma wakazi wa Arusha
pamoja na wateja wao waishio Arusha.
Alisema Dr. Frida, Bima ni muhimu sana kwa kila
binadamu hasa katika maisha ya sasa yenye mlipuko wa
magonjwa mengi, nifulsa yenu sasa wakazi wa Arusha
kutumia nafasi hii.
Nae Meneja wa Resolution Insurance Tanzania, Oscar
Osir alisema wamejipanga vizuri katika kutoa huduma hii
ya Bima ya Afya kwa watanzania nchini kote na sasa
wako katika hatua ya kusogeza huduma hii kila mkoa ndio
maana sasa wamesogea Arusha.
Oscar alisema ni nafasi ya pekee sasa wakazi wa Arusha
kutumia fursa hii ya Bima ya Afya kutoka Resolution
itakayohakikisha kukupa huduma stahiki na nzuri zaidi.
Resolution Insurance ni Kampuni pekee ya Bima ya Afya
inayoongoza East Afrika.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dr.Frida Mokiti(wa pili
kulia) akikata utepe wakati wa ufunguzi wa Tawi jipya la
Bima ya Afya ya Kampuni ya Resolution Insurance jijini
Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Kampuni
hiyo chini, Oscar Osir na Meneja wa Tawi wa la Arusha,
Lucas Msomi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dr.Frida
Mokiti(kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni
ya Bima ya Afya ya Resolution Insurancena pamoja na
wageni waalikwa wakati wa ufunguzi tawi jipya la Kampuni
hiyo katika jingo la NSSF Mafao House mwishoni mwa
wiki mkoani Arusha.
Meneja wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution
Insurance, Oscar Osir(kulia) akizungumza na wageni
waalikwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati
wa ufunguzi wa tawi jipya la Kampuni hiyo jijini Arusha
mwishoni mwa wiki.

No comments:
Post a Comment