Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kangi Lugola (Mbunge wa Mwibala), Mh. Sadiq Murad (Mbunge wa Mvomero) pamoja na Mh. Victor Mwambalaswa (Mbunge wa jimbo la Lupa) wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, kwa kusikiliza kesi inayowakabili ya kushawishi kupatiwa rushwa ya Mil. 30 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja hapa nchini. Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), na wameachiwa kwa dhamana ya sh. mil. 5 kila mmoja na Kesi yao itasikilizwa tena Aprili 14, 2016.
Thursday, March 31, 2016
Home
Unlabelled
WABUNGE WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA
WABUNGE WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment