| Marehemu Balozi Joseph Rwegasira |
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Msasani Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 06 Machi, 2016 mwili wa Marehemu Balozi Rwegasira utaagwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter Mbuyuni saa 8.00 mchana.
Aidha, tarehe 07 Machi, 2016 mwili wa Marehemu utasafirishwa kulekea Bukoba, Kagera kwa mazishi. Wizara inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dar es Salaam
04 Machi, 2016

No comments:
Post a Comment