HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 18, 2016

SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA WANAWAKE - WAZIRI UMMY MWALIMU

Na Mwandishi Maalum, New  York

Wajumbe wa  Mkutano wa 60 wa Kamisheni  kuhusu hali ya wanawake,  wanaendelea na majadilino juu ya   dhima ya  uwezeshwaji wa wanawake na uhusiano wake katika  utekelezaji wa Malengo  ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030).

Akichangia   majadiliano hayo,Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb) anasema  Tanzania  inatambua kwamba uwezeshwaji wa mwanamke na mtoto wa kike ni muhimu sana katika kufanikisha utekelezaji wa   Agenda 2030.

Na kwamba ili  kufanikisha  hilo, Serikali  inaendelea na  jukumu la  kuhusisha na kuingiza   Ajenda 2030  katika  mifumo   iliyopo ya  kisera, mipango na mikakati ya kitaifa ya maendeleo.

Waziri Ummy Mwalimu anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu, amebainisha  pia kwamba  Serikali inapitia kwa makini  lengo namba tano la agenda 2030 ambalo linazungumzia umuhimu wa kufanikisha  usawa wa kijinsi na  uwezeshaji wa wanawake wote na wasichana.

Akaeleza zaidi kwamba uamuzi wa serikali kufanya marejeo ya mikakati  Na mipango ya kitaifa  inalenga kuhakikisha kwamba  usawa wa  jinsia  na uwezeshwaji wa wanawake unaendelea kuwa kipaumbele cha nchi.

Vilevile  amesema,  ushiriki  jumuishi umefanyika katika  kubuni viashiria ambavyo vinaendana na mahitaji ya nchi na vinaweza kutumika  mpaka ngani za chini katika  upimaji wa utekelezaji wa Agenda 2030.

Katika kuelezea  zaidi uzoefu wa Tanzania katika uwezeshwaji wa  mwanamke na msichana wa  kitanzania. Waziri pia alianisha sheria mbalimbali zinazolimda mwanamke na mtoto wa kike dhidi ya  ukatili au ubaguzi wa aina yoyote ile ,  kuanzishwa kwa mifuko na Banki za kuwawezesha wanawake kujipatia mikopo kwa riba nafuu, uboreshwaji wa huduma za afya hususani  afya ya mama na mtoto pamoja na  fursa sawa za ajira zenye staha na fursa za kujiajiri.

Pamoja na kueleza  namna  Serikali inavyoendelea kujipanga katika utekelezaji wa  Agenda 2030,  Waziri Mwalimu amesema ili  utekelezaji huo uwe na  mafanikio  tarajiwa,  ushirikiano na wadau  mbalimbali wa maendeleo pamoja sekta binafsi  utahitajika sana. Na akatumia  nafasi hiyo kuwashukuru wadau hao ambao wamekuwa wakishirikiana na  Serikali   katika maeneo mbalimbali.

Baadhi ya  changamoto ambazo amesema Tanzania inakumbana nazo katika   jukumu hilo la uwezeshwaji wa wanawake na wasichana pamoja na vikwazo vya kimila na kitamadani anavyokumbana navyo mwanamke na  mtazamo hasi dhidi ya wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad