HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 19, 2016

Makonda kuwapa motisha Askari Polisi, awapa siku 90 raia wanaomiliki silaha

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro pamoja na Askari Polisi wa jijini humo kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo, ambapo wamekubaliana kwa pamoja kutoa zawadi ya milioni moja kila baada ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi. 

 "Askari wetu wanafanya kazi katika mazangira magumu na wanachangamoto kubwa. Nimeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha. 

 Akiendelea kuzumza, RC Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanaomiliki silaha, kuziwasilisha silaha zao hizo kwenye ofisi za Jeshi la Polisi ili kufanyiwa ukaguzi, na ametoa muda wa siku 90 kwa mamiliki hao kufanya hivyo.

Aidha amewataka watu wote wanao miliki silaha hizo kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa Oparesheni ya ukaguzi jijini hapa Julai mosi mwaka huu. 

 "Kuna watu wengi wana silaha halali na wengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao.

 "Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu. "Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad