HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 22, 2016

DMF YAANDAA WARSHA YA MANESI WA WODI ZA NJITI TANZANIA

Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) imeandaa semina ya kwanza na ya aina yake nchini kwa Wauguzi wa Wodi za Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti)  Machi 21-22, 2016 kwenye hoteli ya Giraffe ocean View jijini Dar es salaam. 

Doris Mollel Foundation ilizinduliwa Machi 20, 2015. Semina hii imedhaminiwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Asas dairies, GSM Foundation, Kilimanjaro water na Waziri Angela Kairuki ambaye alizaliwa njiti pia.

Dhima ya semina hii ni kuwajengea manesi nchini uwezo wa kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto njiti pamoja na mbinu mbali mbali za kuzuia uzazi wa njiti ambapo  kulingana na takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, takriban watoto 88,128 walizaliwa njiti au wakiwa na uzito mdogo nchini Tanzania mwaka 2014/2015 pekee.

Pamoja na semina hii, DMF kwa kushirikiana na mashirika wadhamini pia wametoa msaada wa mashine 5 za Oxygen zenye thamani ya Tsh 10.3 zilizotelewa na benki ya Amana pamoja na GSM Foundation.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akipokea mashine tatu maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), zilizotolewa na Kampuni ya GSM Foundation, katika Semina ya kuwajengea uwezo Wauguzi nchini wa kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) pamoja na mbinu mbali mbali za kuzuia uzazi wa njiti, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Giraffe ocean View jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa DMF, Dorice Molel ambaye ndie muandaaji wa semina hiyo.

Asasi na makampuni mbalimbali ambao ni washirika wa DMF wamehudhuria warsha hii kuendelea kujionea changamoto mbali mbali ambazo manesi wanakabiliana nazo ili kwa pamoja kuendelea kuona jinsi ya kuwasadia katika kupunguza tatizo hili. Baadhi ya asasi hizi ni Vodacom Foundation, Bank M, Clouds Media Group,  Amana Bank, NSSF, CBA, NHIF, Kilimanjaro Water, Mashirika ya UNICEF, MAMAYE,  JHIPEGO, USAID, TICA, Ubalozi wa Vietnam, Hassan Maajar Trust. Elizabeth Glasier pediatric aid Foundation, FHI360, Plan International, ubalozi wa Japan.

Semina hii ambayo imeongozwa na wataalam wa afya kutoka shirika la kijerumani la GIZ kwa kushirikiana na Dk Augustine Massawe kutoka hospitali ya taifa ya muhimbili imehudhuriwa na manesi (Ma-incharge) kutoka wodi za njiti katika hospitali kuu za mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani na imezinduliwa na Mgeni rasmi Mh Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia katika Semina ya kuwajengea uwezo Wauguzi nchini wa kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) pamoja na mbinu mbali mbali za kuzuia uzazi wa njiti, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Giraffe ocean View jijini Dar es salaam.

Ndani ya mwaka mmoja DMF kwa kushirikiana na wadhamini na washirika mbali mbali imeweza kutoa kufikisha mchango kwenye jamii kwa kuleta  uelewa na mwamko kuhusu tatizo la njiti lakini pia DMF imeweza kufikisha mashine na michango yenye thamani ya Tsh 152,000,000/= (Mia moja na hamsini na mbili milioni) kwenye hospitali 15 nchini pamoja na sekta ya elimu.

DMF Inaishukuru wizara ya Afya pamoja na wadhamini mbali mbali kama Vodacom Foundation, Bank M, Clouds Media Group, Hyatt Regency, NSSF, CBA, NHIF, Coca Cola, Moments productions, UTT AMIS, Ashton Media, iPrint, Bakhresa Group of companies,  Mo Dewji Foundation, Expo Trading, Viva towers, Spik n’ Span, Easy Talk, SpiceNet, Asas Dairies ambao kwa mwaka mzima  wameendelea kufanikisha shughuli hizi.

Mtanzania yeyote pia unaweza kuchangia kupitia M-PESA namba ya kampuni 244444 (Doris Mollel Foundation). Mchango wako wa kiasi chochote kuanzia sh 500/= utasaidia kukusanya fedha zitakazowezesha kununua vifaa kwa hospitali nyingi zaidi nchini.
Sehemu ya washiriki wa Semina hiyo, wakiwemo wadau kutoka tasnia mbali mbali nchini.
Dkt. Massawe akiwasilisha mada kwenye Semina hiyo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad