Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam (Dawasco) Mhandisi Pascal Fumbuka akionyesha moja ya laini ya Maji iliyounganishwa kiholela (wizi wa nyoka) ambapo iliunganishiwa kwenye tenki la kuhifadhi Maji kwa ajili ya kuuza kwa wananchi kwenye eneo la mtaa wa mkundunge Sinza Tandale Jijini Dar es salaam.
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) limebaini wizi mkubwa wa Maji
ujulikanao kwa jina maarufuu kamaa wizi wa nyoka kwenye mitaa ya chama pamoja na mkundunge
Sinza Tandale Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye tukio hilo wakati wa operesheni maalum ya kubaini wizi wa Maji meneja wa
Dawasco Magomeni Mhandisi Pascal Fumbuka amesema kuwa wamebaini wizi mkubwa wa Maji
ujulikanao kwa jina la wizi wa nyoka ambapo wananchi wamejitengenezea laini za Maji kinyemela kwa
kutumia mipira yakawaida na kutoa maji kutoka umbali mrefu nakuzipitisha kwenye nyumba zao au
kuunganisha kwenye tenki za Maji nakuuza bila kibali kutoka Dawasco.
“Leo tumebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kama wizi wa nyoka kwenye mitaa ya Sinza tandale
ambapo wananchi wamekuwa wakijunganishia laini za Maji kwa kutumia mipira ya kawaida kutoka
umbali mrefu nakupitisha kwenye maeneo ya makazi kinyemela bila kupata kibali kutoka Dawasco”,
alisema Fumbuka.
Pia Mhandisi Fumbuka amesema wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa laini zote za Maji
kwa sababu za kiafya ,kutoa elimu kwa wakazi hao yakuwa hawaruusiwi kujiunganishia wenyewe bali
wafike kwenye Ofisi za Dawasco kuomba huduma hiyo na waweze kuwekewa kihalali kwani kuna
ongezo kubwa la Maji jijini hivyo hamna haja ya kuiba Maji ila pia hatua nyingine ni pamoja na
kuwawekea kizimba (kioski) cha Maji ilikuwezesha wakazi hao kuendelea kupata huduma ya Maji.
“Baada ya kubaini wizi wa Maji kwenye mitaa ya Sinza Tandale tumechukua hatua kadha ikiwemo
kuondoa laini zote zilizounganishiwa kinyemela kwa sababu za kiafya kwani laini nyingine zimepita
kwenye bomba za Majitaka , kutoa elimu kwa wakazi kuwa kuna ongezeko la Maji hivyo mtu yeyote
anayehitaji huduma ya Maji afike kwenye ofisi zetu za Dawasco tuweze kumuunganishia kihalali pia
tumeweka kizimba cha Maji kitakacho toa huduma ya Majisafi ilikuwezesha wakazi waendelee kupata
huduma ya Maji kama kawaida”,alisema Fumbuka.
Kwa upande wawakazi wa Sinza Tandale akiwemo Mzee Seif Shabani Mohamed amekiri kuwepo kwa
wizi mkubwa wa Maji kwenye mitaa hiyo nakusema kuwa unatokana na gharama kuwa kubwa za
kuunganishiwa huduma ya Maji pamoja na ubabaishaji kuwa mkubwa ukiomba huduma hiyo hivyo
ameiomba Dawasco kupunguza gharama za kuunganishiwa Maji ilikufanya wakazi wenye kipato cha
cha chini kumudu gharama itasaidia kupunguza tatizo la wizi wa Maji kwani wananchi wengi
watajiunganishia kihalali.
“Kweli mitaa mingi hapa Tandale kuna tatizo la wizi wa Maji ila inatokana na gharama kubwa ya ada ya
kuunganishiwa huduma ya Maji na pia ukiomba kuunganishiwa mchakato unakuwa una ubabaishaji
mrefu hivyo kufanya wananchi wenye kipato cha chini kutoweza kumudu gharama pamoja na kukata
tama kutokana ubaishaji ila gharama zikipunguzwa itasaidia kupunguza tatizo la wizi wa Maji”, alisema
Mzee Seif.
Dawasco inaendelea kuwasihi wakazi wote wa Jiji la Dar es salaam kuepuka kujiunganishia huduma
ya Maji kinyemela kwani operesheni ya kubaini wezi wa Maji kwenye maeneo mbalimbali ya jiji ni
endelevu na pia ni agizo kutoka kwa waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge pamoja na Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambao waliagiza Dawasco kuwabaini wezi wa Maji
hivyo wale wote waliojiunganishia bila kibali kutoka Dawasco wajisalimishe iliwaweze kupewa kibali
halali kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika akitumia huduma ya
Maji kwa wizi.



No comments:
Post a Comment