JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
· MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KUGONGANA JIJINI MBEYA.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WAWILI WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 KWA MAKOSA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA [DEREVA] WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 321 CSV AINA YA TOYOTA COASTER AITWAYE LWIMIKO MWANSASU [36] MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 877 CWE AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA SUPERSHEM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL JOHN [42] MKAZI WA MWANZA KUGONGANA NA GARI HILO NA KISHA KULIGONGA GARI JINGINE LENYE NAMBA ZA T. 321 CSV AINA YA TOYOTA HIACE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAKISYE MBOMA [45] MKAZI WA AIRPORT.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO ENEO LA SOWETO, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA BASI HILO LILILOKUWA LINATOKA MBEYA KUELEKEA MWANZA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA 1. AYNO ASATA [21] NA 2. CHARU SUMESO [18] KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA MAJENGO, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO 1. HAIDAN RODRICK [35] 2. JULIUS BUTEMELE [53] 3. VISENT MAPILE [29] 4. DOTO MWASHITETE [25] NA 5. JOSEPH BUTEMELE [40] WOTE WAKAZI WA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].
WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ISANGAWANA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTU MMOJA MKAZI WA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMANNE HAONGA [32] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 11:20 ASUBUHI HUKO KIJIJI, KATA NA TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
MTU MMOJA MKAZI WA ILOLO WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DANIEL NZUNDA [30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 13:40 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ILOLO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA ZA KUINGIA NCHINI ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment